22 September, 2014

MAWAZO YANGU

Ili kuongeza uwezo wa vijana kujiajiri,wanafunzi wa elimu ya juu wajisomeshe wenyewe,baada ya kuhitimu ndipo wapatiwe mkopo,ambayo itasaidia wao kujiajiri. Faida zake:- ¤wanafunzi watajiajiri na kuweza kuajiri watu wengine. ¤kutakuwa urahisi na uhakika wa pesa za serikalikurudishwa ili iweze kusaidia na wengine. ¤itaongeza hamu ya wanafunzi kusoma na kufaulu kitaalamu na kitaaluma kwani watajua wanakwenda kuitumia elimu atakayoipata kwa manufaa yake mwenyewe,hivyo taifa kwa ujumla. ¤uchumi wa taifa utakuwa kutokana na pesa itakayotolewa kwa ajiri ya mikopo ya wanafunzi itakuwa kwenye mzunguko kwani itakopwa na kurudishwa kwa uhakika tofauti na sasa kwani ufuatiliaji utakuwa ni rahisi hivyo kuweza kukopesha wanafunzi wengine badala ya kutenga fungu jipya kila mwaka,hii itasaidia serikali kwani itaokoa pesa nyingi na kuweza kusaidia sekta ya elimu.

No comments:

Post a Comment